Genesis 5

Kutoka Adamu Hadi Nuhu

(1 Nyakati 1:1-4)

1 aHii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu.

Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.
2 bAliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”

3 cAdamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. 4Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 5 dAdamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.

6 eSethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. 7Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 8Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.

9 fEnoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 11Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.

12 gKenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 14Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.

15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 17Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

18 hYaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Idrisi. 19Baada ya kumzaa Idrisi, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 20Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.

21 iIdrisi alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22 jBaada ya kumzaa Methusela, Idrisi alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 23Idrisi aliishi jumla ya miaka 365. 24 kIdrisi akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

25 lMethusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki. 26Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 27Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.

28Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. 29 mAkamwita jina lake Nuhu, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.” 30Baada ya Nuhu kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 31Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.

32 nBaada ya Nuhu kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.
Copyright information for SwhKC